Thursday, 31 January 2013

WENYE BODABODA MTIBWA WALIA NA TRA



Waendesha Boda Boda wakilalamikia na kujadili vitendo vya kodi na kukamatwa ovyo.

Na. Bryceson Mathias, Mvomero

Madereva na Wamiliki wa Pikipiki maarufu kwa Jina la Bodaboda, wameilalamikia Mamlaka ya Mapato (TRA) Mji Mdogo wa Madizini na Kampuni ya Udalali ya MEM Auction Mart, wakiituhumu kuwanyanyasa na na wakati mwingine kuwadai Rushwa wanapofanya kazi yao ya kuwakagua na kukamata vyombo vyao.

Malalamiko hayo yalitolewa na Wadau jana kufuatia kuwepo kwa kamata Kamata ya Ukaguzi dhidi ya Uhalali wa Vyombo hivyo, iwepo vmetimiza masharti yote yanatpaswa kutimizwa ili viweze kutumika  kuwahudumia wananchi bila kuwa na kasoro zinazoweza kusababisha matatizo miongoni mwa Jamii.

Baadhi ya Wenye Vyombo na Madereva waliokaguliwa walidai kwamba, pamoja na kuwa na Vielelezo vinavyostahili kuwa navyo, kuna akati walilazimishwa kuwasilisha vyote kwa wakati huo na kutakiwa kuacha vyombo vyao hapo, na kutishiwa kama vikilala watalazimika kulipia Shilingi 20,000/- kila Chombo jambo walilodai ni kuwanyanyasa.

“Tulikamatwa na kutakiwa kuwasilisha nyaraka zote hata zile ambazo zinatakiwa kutunzwa nyumbani, wamedai walisumbuliwa kiasi kubaini kwamba wanafanyiwa hivyo ili yu mkini kuwalazimisha atoe chochote ili waondoke na wengine kudai walilfikia kudaiwa Shilingi 10,000/- Ili waachiwe”.alisema mmoja wao aliyeombwa asitajwe jina.

Ofisa wa TRA Mji Mdogo wa Madizini, Salum Mwanamsha alipoulizwa kuhusu Malalamiko hayo alisema, Kazi ya Ukaguzi wa vyombo hivyo haifanywi na TRA bali kuma Kampuni ya Udalali ya Mem ambapo dai la kuwepo kwa harufu ya rushwa hawezi kuisemea.

Mmoja wa watendaji mwenye Namba ya Simu 0715-413736 alimwandikia mwandishi ujumbe mfupi kati ya jumbe mbili za vitisho ukisema,  

“Naomba umlete huyo au ww kuhusu tuhuma ya kutoa elfu 10 ili pikipiki itoke, maana hiyo piikipiki ameitoa Salum wakati mm sina ruhusa ya kutoa name nimesikitishwa na tuhuma mnanizushia na swla hili nitalifikisha mbele ya sheria naijua pikipiki ninamtafuta aje athibitishe kauli mnazonizitoa”

Awali Wananchi wenye vyombo wakiwemo Madereva wa Bodaboda walilalamika kwamba, ‘Pamoja na Dereva wao ambaye ni Mkuu wa Msafara katika kukamata Pikipiki, walikuwa wanaingia hadi ndani Chumbani wakiwa na Polisi mwenye Bundukisema, jambo ambalo lilionekana kuwaudhi watendewa na kulitolea malalamiko’.

No comments: