Thursday, 31 January 2013

KIPAWA YAZINDUA MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA AWAMU YA PILI

Kata ya Kipawa iliyopo katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, imezindua rasmi Mpango Kabambe wa kuboresha Mazingira katika kata hiyo kwenye Shule, Mpango unaokwenda kwa jina la Mazingira Bora kwa Elimu Bora Awamu ya Pili kwa wenye Kipawa.
 Uzinduzi huo umefanyika leo katika Shule ya Msingi Minazi Mirefu iliyopo Ukonga Jijini Dar es Salaam, ambapo katika uzinduzi huo wakazi wa Ukonga wametakiwa kuchangia tofali mojamoja kwa kila mwana kipawa ambapo watalipia shilingi 1000 kila mmoja zitakazo saidia kununua Matofali ya Kujenga choo katika Shule hiyo ambayo kwa sasa ina Matundu Mawili tu.

Akizungumza katika Uzinduzi wa Mpango huo, Diwani wa Kata ya Kipawa Mhe, Bonnah Kaluwa, amesema kuwa Mpango huo utasaidia kuweka mazingira ya kata hiyo katika hali ya Usafi ambapo itaboresha afya za wakazi wa Kipawa.

Diwani Kaluwa amesema kuwa Mpango huo unadhaminiwa na watu wa Marekani lakini Dhamana itaanza baada ya jitihada ya wakazi wa Kipawa kuonekana.

Kwa upande wake Ofisa Utamaduni Msaidizi katika Ubalozi wa
 Marekani, Bi, Shamsa Suleiman amesema kuwa wapo tayari kusaidia Kuboresha Mazingira Bora kwa Elimu katika kata hiyo.


Diwani wa Kata ya Kipawa Mhe, Bonnah Kaluwa kulia pamoja na Ofisa Utamaduni katika Ubalozi wa Marekani Bi, Shamsa Suleiman, wakihesabu pesa zilizochangwa na wananchi wa kata hiyo kwa ajili ya Kununua matofali ya kujengea choo katika Shule hiyo ya Minazi Mirefu.

Diwani wa Kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa akitoa neno  fupi katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo
Ofisa Utamaduni Msaidizi katika Ubalozi wa Marekani,  
Shamsa Suleiman, akitoa neno fupi katika uzinduzi huo. 
Marekani imeonesha nia ya kufadhili mradi huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Minazi Mirefu, 
Daniel Mwamasika, akiwasalimia wananchi na wageni 
waalikwa waliofika katika uzinduzi huo.
Diwani ya Kata hiyo Bonnah Kaluwa, akiwasili katika 
uzinduzi huo uliofanyika leo. Kutoka kushoto ni Ofisa 
Utamaduni Msaidizi katika Ubalozi wa Marekani,  
Shamsa Suleiman na  Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo 
Said Fundi
Diwani wa Kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa (katikati), akizungumza na wananchi wa kata hiyo wakati wa 
hafla ya uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa Mazingira
 Bora kwa  Elimu Bora. Hafla hiyo  ilifanyika Shule ya  Msingi Minazi Mirefu Ukonga Dar es Salaam leo. 
Mradi huo unafadhiliwa na nchi ya Marekani. Kushoto
 ni Ofisa Utamaduni Msaidizi katika Ubalozi wa  Marekani,  Shamsa Suleiman na Kushoto kwa Diwani 
huyo ni 
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Minazi 
Mirefu, 
Daniel Mwamasika.

No comments: