Thursday, 31 January 2013

DC MVOMERO AWAKOROMEA WAFUGAJI, WAHAME KABLA YA KUHAMISHWA



MKUU wa Wilaya ya Mvomero Antony Mtaka, amewakoromea na kuwataka wafugaji waliovamia na kuhamia Katika Vijiji vya Kata ya Mtibwa wilayani humo bila vibali, kuhama wenyewe mara moja kabla sheria ya kuwahamishwa kwa nguvu haijachukua Mkondo wake.

Mtaka aliyasema hayo mwanzoni mwa wiki katika Kijiji cha Kunke kutokana na kuwepo uvamizi Holela katka Vijiji vya Kunke, Kunke, Kisala, Lukenge Kijijini, Lungo, Mlumbilo, Dihinda na hasa vitongojo vvya Ndavindavi kiasi cha mifugo yao kuharibu mazao ya wakulima hivyo kutishia kuwepo kwa Njaa.

Akizungumza na Wananchi na Viongozi wa Kijiji cha Kunke Sambamba na Viongozi wa Kata ya Mtibwa, Mtaka aliwataka Wafugaji waliovamia na kuhamia katika maeneo ya Kilimo vijijiji kinyelmela na kutishia Ustawi wake, Wachukue hatua ya kuhame wenyewe mapema, kabla ya sheria ya kuwahamisha kwa nguvu ili kulinda Ustawi huo, haijachukua Mkondo wake.

“Ni vema wafugaji waliovamia maeneo ya Kilimo, wachukue hatua ya kuhama wenye kabla ya hatua ya kuwahamisha kwa nguvu ili kulinda ustawi wa Kilimo cha Mazao yaliyomo mashambani hivi sasa, hazijachukuliwa”.alisema Mtaka.

Aidha aliwataka Viongozi na Watendaji wote kuhakikisha suala hilo linafanyika kwa Amani bila kuathiri Mazao yaliyomo mashambani, ukizingatia kuharibiwa kwa mazao yalipandwa na kuota hivi sasa kutakuwa kunatishia hali ya Chakula wilayani humo.

Hatua ya Mtaka inajibu Kilio cha Wakazi wengi wa Wilaya ya Mvomero, Tarafa, Kata, Vijiji na Vitobgoji vyake kutokana na kuwepo kwa Vurugu za Wafugaji na Wakulima ambapo wakulima walikuwa wanalalamikia mazao yao kulishwa na Wafungaji hivyo kuharibu ustawi wa Chakula kwa maisha yao.

Hata hivyo Katika Vurugu hizo, Diwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Athumani Mkimbu, aliwahi kujeruhiwa na wafungaji hao kiasi cha kushonwa zaidi Nyuzi 12, ambapo Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kisala Shija Msafiri wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), naye aalijeruhiwa kicha na kushonwa nyuzi Nane na wananchi wengine kujeruhiwa vibaya.

No comments: