Thursday 31 January 2013

KIM ATEUA 21 STARS WA KUIVAA CAMEROON


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen (pichani) ametaja kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia kambini Jumapili (Februari 3 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Cameroon (Indomitable Lions).
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo, Kim amesema mechi dhidi ya Cameroon itakuwa kipimo kizuri kwake kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayofanyika Machi mwaka huu.
 
“Itakuwa mechi ngumu na kipimo sahihi kwetu. Tuko tayari, tutacheza kwa staili yetu kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya mechi dhidi ya Morocco. Ni mechi nzuri kwa sababu wachezaji wameonyesha wako tayari.
 
“Tumetoka kucheza dhidi ya Zambia na Ethiopia. Lengo ni Taifa Stars kucheza fainali za AFCON 2015, kwa hiyo mechi dhidi ya Cameroon ni sehemu ya mipango yetu kuhakikisha tunafika huko,” amesema Kim ambaye amerejea nchini juzi kutoka Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Morocco na Ivory Coast zilizo kundi moja na Tanzania katika mechi za mchujo za Kombe la Dunia.
 
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco, Machi 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars inashika nafasi ya pili katika kundi lake nyuma ya Ivory Coast inayoongoza. Timu nyingine katika kundi hilo ni Gambia.
 
Wachezaji aliowaita kwenye kikosi chake ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar).
 
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), na Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
 
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

KIPAWA YAZINDUA MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA AWAMU YA PILI

Kata ya Kipawa iliyopo katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, imezindua rasmi Mpango Kabambe wa kuboresha Mazingira katika kata hiyo kwenye Shule, Mpango unaokwenda kwa jina la Mazingira Bora kwa Elimu Bora Awamu ya Pili kwa wenye Kipawa.
 Uzinduzi huo umefanyika leo katika Shule ya Msingi Minazi Mirefu iliyopo Ukonga Jijini Dar es Salaam, ambapo katika uzinduzi huo wakazi wa Ukonga wametakiwa kuchangia tofali mojamoja kwa kila mwana kipawa ambapo watalipia shilingi 1000 kila mmoja zitakazo saidia kununua Matofali ya Kujenga choo katika Shule hiyo ambayo kwa sasa ina Matundu Mawili tu.

Akizungumza katika Uzinduzi wa Mpango huo, Diwani wa Kata ya Kipawa Mhe, Bonnah Kaluwa, amesema kuwa Mpango huo utasaidia kuweka mazingira ya kata hiyo katika hali ya Usafi ambapo itaboresha afya za wakazi wa Kipawa.

Diwani Kaluwa amesema kuwa Mpango huo unadhaminiwa na watu wa Marekani lakini Dhamana itaanza baada ya jitihada ya wakazi wa Kipawa kuonekana.

Kwa upande wake Ofisa Utamaduni Msaidizi katika Ubalozi wa
 Marekani, Bi, Shamsa Suleiman amesema kuwa wapo tayari kusaidia Kuboresha Mazingira Bora kwa Elimu katika kata hiyo.


Diwani wa Kata ya Kipawa Mhe, Bonnah Kaluwa kulia pamoja na Ofisa Utamaduni katika Ubalozi wa Marekani Bi, Shamsa Suleiman, wakihesabu pesa zilizochangwa na wananchi wa kata hiyo kwa ajili ya Kununua matofali ya kujengea choo katika Shule hiyo ya Minazi Mirefu.

Diwani wa Kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa akitoa neno  fupi katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo
Ofisa Utamaduni Msaidizi katika Ubalozi wa Marekani,  
Shamsa Suleiman, akitoa neno fupi katika uzinduzi huo. 
Marekani imeonesha nia ya kufadhili mradi huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Minazi Mirefu, 
Daniel Mwamasika, akiwasalimia wananchi na wageni 
waalikwa waliofika katika uzinduzi huo.
Diwani ya Kata hiyo Bonnah Kaluwa, akiwasili katika 
uzinduzi huo uliofanyika leo. Kutoka kushoto ni Ofisa 
Utamaduni Msaidizi katika Ubalozi wa Marekani,  
Shamsa Suleiman na  Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo 
Said Fundi
Diwani wa Kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa (katikati), akizungumza na wananchi wa kata hiyo wakati wa 
hafla ya uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa Mazingira
 Bora kwa  Elimu Bora. Hafla hiyo  ilifanyika Shule ya  Msingi Minazi Mirefu Ukonga Dar es Salaam leo. 
Mradi huo unafadhiliwa na nchi ya Marekani. Kushoto
 ni Ofisa Utamaduni Msaidizi katika Ubalozi wa  Marekani,  Shamsa Suleiman na Kushoto kwa Diwani 
huyo ni 
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Minazi 
Mirefu, 
Daniel Mwamasika.

Dk. Migiro afanya ziara wilaya mpya ya Buhigwe Mkoani Kigoma

Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea maeneo hayo na kuweza kujionea changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo wananchi hao ikiwa ni pamoja na kutembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Soko la Kimataifa litakalowanufaisha wakazi wengi wa wilaya hiyo ambao wako kando kando ya Mto Maragarasi unaopakana na nchi jirani ya Burundi.Dkt. Migiro pia amewaasa wananchi wa maeneo hayo kuwa na umoja,mshikamano na upendo ili kuweza kuhimarisha mambo mbali mbali ya Wilaya.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Buhigwe ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akicheza ngoma ya asili ya kabila la Waha waliokuja kumpokea.
Wananchi wa Kijiji cha Buhigwe wakimuaga Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa CCM katika Kijiji cha Mnanila,Wilayani Buhigwe.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Mnanila kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati akiendelea na Ziara yake ya kutembelea Kata zote zilizopo wilayani humo.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Buhigwe ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwapungia watoto wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma mara baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa Kijiji hicho jana.
Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Buhigwe ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wakimsikiliza Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro aliekuwa kwenye Ziara ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe,Ndg. Gishuli Mbegesi (kulia) akikabidhi Taarifa ya Utekelezani wa Ilani ya Uchaguzi kwa Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akipokea ripoti ya Chama Wilaya ya Buhigwe,kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Buhigwe,Bi. Bennosa Mjema.Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo,Ndg. Elisha Bagwanya
Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Buhigwe wakimsikiliza Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro aliekuwa kwenye Ziara ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akicheza ngoma ya asili ya kabila la Waha sambamba na Bibi Buchiro Edmas Kapina wakati wa Ziara ya kutembelea wilaya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akilakiwa kwa shangwe na kinamama wa Kijiji cha Kilelema.
Mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Kilelema,Everist Samson akisoma taarifa ya kijiji kuhusiana na changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi wa kijiji hizo zikiwemo zile za kuvamiwa na majambazi wanaotoka nchi jirani ya Burundi.Kijiji hiki kipo mpakani kabisa mwa Tanzania na Burundi kwa kijiji cha Buhema Mkoani Lutana,nchini Burundi.
Wananchi wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakimsikiliza kwa makini Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro (hayupo pichani).
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilelema,Benedict Samson Mahuta (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya eneo la Soko kwa Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro (katikati),alietembelea eneo litakalojengwa soko la Kimataifa katika Kijiji hicho cha Kilelema.
Picha ya Pamoja na Watendaji wa Kijiji cha Kilelema.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro (pili kulia) akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe,Ndg. Gishuli Mbegesi Charles (kushoto) kuelekea kwenye eneo la mpaka wa Tanzania na Burundi unaotenganishwa na sehemu ya Mto Maragarasi.

WENYE BODABODA MTIBWA WALIA NA TRA



Waendesha Boda Boda wakilalamikia na kujadili vitendo vya kodi na kukamatwa ovyo.

Na. Bryceson Mathias, Mvomero

Madereva na Wamiliki wa Pikipiki maarufu kwa Jina la Bodaboda, wameilalamikia Mamlaka ya Mapato (TRA) Mji Mdogo wa Madizini na Kampuni ya Udalali ya MEM Auction Mart, wakiituhumu kuwanyanyasa na na wakati mwingine kuwadai Rushwa wanapofanya kazi yao ya kuwakagua na kukamata vyombo vyao.

Malalamiko hayo yalitolewa na Wadau jana kufuatia kuwepo kwa kamata Kamata ya Ukaguzi dhidi ya Uhalali wa Vyombo hivyo, iwepo vmetimiza masharti yote yanatpaswa kutimizwa ili viweze kutumika  kuwahudumia wananchi bila kuwa na kasoro zinazoweza kusababisha matatizo miongoni mwa Jamii.

Baadhi ya Wenye Vyombo na Madereva waliokaguliwa walidai kwamba, pamoja na kuwa na Vielelezo vinavyostahili kuwa navyo, kuna akati walilazimishwa kuwasilisha vyote kwa wakati huo na kutakiwa kuacha vyombo vyao hapo, na kutishiwa kama vikilala watalazimika kulipia Shilingi 20,000/- kila Chombo jambo walilodai ni kuwanyanyasa.

“Tulikamatwa na kutakiwa kuwasilisha nyaraka zote hata zile ambazo zinatakiwa kutunzwa nyumbani, wamedai walisumbuliwa kiasi kubaini kwamba wanafanyiwa hivyo ili yu mkini kuwalazimisha atoe chochote ili waondoke na wengine kudai walilfikia kudaiwa Shilingi 10,000/- Ili waachiwe”.alisema mmoja wao aliyeombwa asitajwe jina.

Ofisa wa TRA Mji Mdogo wa Madizini, Salum Mwanamsha alipoulizwa kuhusu Malalamiko hayo alisema, Kazi ya Ukaguzi wa vyombo hivyo haifanywi na TRA bali kuma Kampuni ya Udalali ya Mem ambapo dai la kuwepo kwa harufu ya rushwa hawezi kuisemea.

Mmoja wa watendaji mwenye Namba ya Simu 0715-413736 alimwandikia mwandishi ujumbe mfupi kati ya jumbe mbili za vitisho ukisema,  

“Naomba umlete huyo au ww kuhusu tuhuma ya kutoa elfu 10 ili pikipiki itoke, maana hiyo piikipiki ameitoa Salum wakati mm sina ruhusa ya kutoa name nimesikitishwa na tuhuma mnanizushia na swla hili nitalifikisha mbele ya sheria naijua pikipiki ninamtafuta aje athibitishe kauli mnazonizitoa”

Awali Wananchi wenye vyombo wakiwemo Madereva wa Bodaboda walilalamika kwamba, ‘Pamoja na Dereva wao ambaye ni Mkuu wa Msafara katika kukamata Pikipiki, walikuwa wanaingia hadi ndani Chumbani wakiwa na Polisi mwenye Bundukisema, jambo ambalo lilionekana kuwaudhi watendewa na kulitolea malalamiko’.

DC MVOMERO AWAKOROMEA WAFUGAJI, WAHAME KABLA YA KUHAMISHWA



MKUU wa Wilaya ya Mvomero Antony Mtaka, amewakoromea na kuwataka wafugaji waliovamia na kuhamia Katika Vijiji vya Kata ya Mtibwa wilayani humo bila vibali, kuhama wenyewe mara moja kabla sheria ya kuwahamishwa kwa nguvu haijachukua Mkondo wake.

Mtaka aliyasema hayo mwanzoni mwa wiki katika Kijiji cha Kunke kutokana na kuwepo uvamizi Holela katka Vijiji vya Kunke, Kunke, Kisala, Lukenge Kijijini, Lungo, Mlumbilo, Dihinda na hasa vitongojo vvya Ndavindavi kiasi cha mifugo yao kuharibu mazao ya wakulima hivyo kutishia kuwepo kwa Njaa.

Akizungumza na Wananchi na Viongozi wa Kijiji cha Kunke Sambamba na Viongozi wa Kata ya Mtibwa, Mtaka aliwataka Wafugaji waliovamia na kuhamia katika maeneo ya Kilimo vijijiji kinyelmela na kutishia Ustawi wake, Wachukue hatua ya kuhame wenyewe mapema, kabla ya sheria ya kuwahamisha kwa nguvu ili kulinda Ustawi huo, haijachukua Mkondo wake.

“Ni vema wafugaji waliovamia maeneo ya Kilimo, wachukue hatua ya kuhama wenye kabla ya hatua ya kuwahamisha kwa nguvu ili kulinda ustawi wa Kilimo cha Mazao yaliyomo mashambani hivi sasa, hazijachukuliwa”.alisema Mtaka.

Aidha aliwataka Viongozi na Watendaji wote kuhakikisha suala hilo linafanyika kwa Amani bila kuathiri Mazao yaliyomo mashambani, ukizingatia kuharibiwa kwa mazao yalipandwa na kuota hivi sasa kutakuwa kunatishia hali ya Chakula wilayani humo.

Hatua ya Mtaka inajibu Kilio cha Wakazi wengi wa Wilaya ya Mvomero, Tarafa, Kata, Vijiji na Vitobgoji vyake kutokana na kuwepo kwa Vurugu za Wafugaji na Wakulima ambapo wakulima walikuwa wanalalamikia mazao yao kulishwa na Wafungaji hivyo kuharibu ustawi wa Chakula kwa maisha yao.

Hata hivyo Katika Vurugu hizo, Diwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Athumani Mkimbu, aliwahi kujeruhiwa na wafungaji hao kiasi cha kushonwa zaidi Nyuzi 12, ambapo Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kisala Shija Msafiri wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), naye aalijeruhiwa kicha na kushonwa nyuzi Nane na wananchi wengine kujeruhiwa vibaya.