Wednesday 1 May 2013

HUYU HAPA MWANAFUNZI WA KIKE MJINGA KULIKO WOTE HUJAPATA KUONA


"Nilicho penda kutoka kwa huyu BOYFRIEND wangu ni kua ananijali sana na ana pesa kwan kwao wanajiweza kifedha... ananionga sana PESA kwani nikitaka hela ya CHIPS KUKU hua ananipa, hela ya lotion, pafyumu na saloon hua ananipa kila mwezi kwahiyo sina shida na shule wala sioni umuhimu wa shule.

NAOMBENI ushauri wenu jamani.. niwaambie nini WAZAZI wangu ili wanikubalie niache SHULE ili niolewe na huyu MWANAUME nifaidi pesa zake na mali za nyumbani kwao...
Hi Admin!!

Mimi naitwa NEEMA ni msichana wa miaka 18 Nasoma kidato cha tatu (form 3) hapa jijini DAR-ES-SALAAM.... nimejitokeza kwenu kuomba ushauri

Mimi nina mpenzi wangu ambae yupo chuo kikuu cha UDSM, ana miaka 25...  kutokana na mapenzi anayo nionyesha sitamani tena kuendelea na shule... kwani nikiwa darasani muda wote namuwaza yeye tu

Nilicho penda kutoka kwa huyu BOYFRIEND wangu ni kua ananijali sana na ana pesa kwan kwao wanajiweza kifedha...  ananionga sana PESA kwani nikitaka hela ya CHIPS KUKU hua ananipa, hela ya lotion, pafyumu na saloon hua ananipa kila mwezi kwahiyo sina shida na shule wala sioni umuhimu wa shule. 

NAOMBENI ushauri wenu jamani..  niwaambie nini WAZAZI wangu ili wanikubalie niache SHULE ili niolewe na huyu MWANAUME nifaidi pesa zake na mali za nyumbani kwao...

MHANDISHI WA MAJI NJOMBE AMEKUTWA AMEFARIKI KATIKA KISIMA CHA MAJI


..

 Kikosi cha Zima moto na uokoaji cha Halmashauri ya mji wa Njombe kwa kushirikiana na wananchi wakitoa mwili wa Mhandisi wa Maji katika Halmashauri ya Mji wa Njombe Abdalah Mgambo baada ya kutumbukia kwenye kisima hicho jana katika Uwanja wa ukumbi wa Turbo Mjini Njombe.
 Mwili wa Eng.Abdalah Mgambo ukionekana kwa umbali kwenye gari la Polisi ukipelekwa hospitali Kibena kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.
 Wa pili kushoto ni Mhandisi wa Maji Halamshauri ya Mji wa Njombe Eng.Abdalah Mgambo enzi za uhai wake wakati wa Kilele cha Wiki ya Maji March 22 mwaka huu katika kijiji cha Igominyi.
Marehemu Abdalah Mgambo enzi za Uhai wake akisoma taarifa ya Hali ya maji katika halmashauri ya Mji wa Njombe mwezi machi 22 mwaka huu wakati wa kilele cha wiki ya Maji Igominyi Njombe.
Taarifa toka eneo la Tukio zinasema kuwa marehemu Abdalah Mgambo alikuwa katika Baa yake eneo la Ukumbi wa Turbo Mjini Njombe kisha akamuaga mke wake kwamba anatoka nje kujipumzisha kwenye gari lake majira ya Saa Moja jioni jana April 30 akatoweka ghafla na kisha Kadi yake ya Benki ya NMB Ilikutwa nje ya Kisima cha Maji kilichopo katika uwanja wa Ukumbi wa Turbo Mjini Njombe.

WAFANYAKAZI SWAFIIII???



Tuesday 2 April 2013

MKASA wa baba kumuua mwanae kwa kumzika akiwa hai kutokana na mgogoro wa ndoa, umezidi kuibua mapya, baada ya mama mzazi wa marehemu ,Debora Riziki (3), kusimulia mkasa mzima .


Marehemu Debora Riziki miaka 3 enzi za uhai wake
Riziki Mwangoka kulia anaetuhumiwa kumzika mtoto wake akiwa hai

Hapa maiti ya mtoto Debora ikiwa imetolewa nnje mara baada ya kufukuliwa ndani ya nyumba ya baba yake mzazi 
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI TUNAZOZIONYESHA

Mwili wa marehemu Debora  ukionyeshwa kwa mzazi na kudhibitisha kuwa ndiye mwenyewe aliyemfukia 
Mwili wa mtoto Debora ukiandaliwa kwa kuzikwa kwa heshima zote
Mwili wa Debora tayari kwa kuzikwa
Hatimae sasa Debora anazikwa
Mara tu baada ya mazishi baba mzazi wa Debora anapelewa kituo cha polisi Tukuyu

Mama mzazi wa marehemu Debora asimulia kisa chote
 Mama mzazi wa Marehemu, Esther Mwambenja, alisema kabla ya tukio hilo kutokea kulikuwa na viashiria vingi vya mumewe kufanya ukatili
Bibi wa marehemu Debora 
Tukiwa na baadhi ya waandishi wenzangu tukiendelea kupata historia fupi ya marehemu Debora toka kwa mama yake mzazi
 Novemba 15 mwaka 2012 serikali ya kijiji chini ya Mwenyekiti, Lutengano Mwakyoma na mashahidi watano wakiwemo wazazi na ndugu zake, walinikabidhi barua ya kuridhia kuondoka na mwanangu, huku ikimuonya mume wangu kutorudia kosa hili la kumuiba mtoto hadi hapo atakafikisha miaka saba.
 Dada wa marehemu Debora, Neema Stevini(5) kulia ambaye ni mtoto wa kufikia wa baba mzazi wa marehemu, akisimulia jinsi mdogo wake alivyoibwa , alisema kuwa anakumbuka mara ya mwisho ilikuwa jioni majira ya saa 12 jioni.
“Nilitaka kwenda nao, lakini baba Debora akaniambia nirudi kuchochea moto ndani na niliporudi nikakuta wameondoka na nilipokimbilia sana siku waona” alisema kwa masikitiko Neema.
Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango akiwaanasindikizwa na dogo Asajile huku akielezwa ni jinsi gani walimfahamu mtoto mwenzao Debora kwakweli watoto hawa wamesema hawaamini kabisa kama Debora hawata mwona tena





MKASA wa baba kumuua mwanae kwa kumzika akiwa hai kutokana na mgogoro wa ndoa, umezidi kuibua mapya, baada ya mama mzazi wa marehemu ,Debora Riziki (3), kusimulia mkasa mzima .
Akizungumza kwa hisia kali, katika mahojiano maalumu  na Mbeya yetu kijijini kwake Ibula, katika kata ya Kiwira, wilayani Rungwe, Mama mzazi wa Marehemu, Esther Mwambenja, alisema kabla ya tukio hilo kutokea kulikuwa na viashiria vingi vya mumewe kufanya ukatili.
Alisema  tukio la mzazi mwenza huyo kumwiba mtoto  na kwenda kumfanyia  ukatili huo wa kinyama lilikuwa la pili, baada ya awali kumuiba akiwa na miaka miwili na miezi mine na alimrudisha kwa maandishi ya serikali ya kijiji.
Alisema katika tukio la kwanza la mtalaka wake huyo kumuiba mtoto wao huyo, lilitokea Septemba mwaka 2012, baada ya wiki chache za kumfukuza katika nyumba waliyokuwa wakiishi katika kitongoji cha Iponjola, kijiji cha Asenga, nyumba iliyotumika kuzikwa mtoto huyo.
Alitaja sababu za yeye kufukuzwa ni ugomvi uliotokana na yeye kuhoji  sababu za kuficha fedha kiasi cha sh. 120,000 zilizotokana na wao  kwa pamoja kufanya  kazi ya kibarua katika mashamba kijijini hapo na baada ya malipo kutolewa mtalaka wake huyo alionesha kiasi kidogo cha sh.80,000.
Alisema ugomvi huo ndio ulisababisha  yeye arudishwe kwa wazazi wake, lakini baada ya muda mfupi mwanaume huyo  alimfuata na kumbembeleza ili warudiane na alipogoma aling’ang’ania aondoke na mtoto .
“Nakumbuka ilikuwa Novemba mwaka jana baada ya mimi kuondoka nyumbani kwake na kurudi kuishi hapa nyumbani, siku hiyo tukiwa shambani huyo bwana alikuja hapa nyumbani na kumkuta mwanangu wa kwanza (Neema Steven ) niliyezaa na mwanaume mwingine” alisema Mwambenja.
Alisema baada ya kufika eneo hilo majira ya saa mbili asubuhi alitumia ujanja na kufanikiwa kumuiba mtoto na kisha kutokomea naye kijijini kwao Asenga, hali ambayo ilisababisha kutoa taarifa kituo cha polisi Kiwira.
“Unajua kuwa baada ya kwenda kutoa taarifa polisi walitusaidia kufika kijijini kwao ambapo serikali ya kijiji ilikubali nimchukue mwanangu kwa kuwekeana mkataba wa kisheria kwa mujibu wa sheria, kwani alikuwa chini ya miaka saba”.
Aliongeza kuwa  Novemba 15 mwaka 2012 serikali ya kijiji chini ya Mwenyekiti, Lutengano Mwakyoma na mashahidi watano wakiwemo wazazi na ndugu zake, walinikabidhi barua ya kuridhia kuondoka na mwanangu, huku ikimuonya mume wangu kutorudia kosa hili la kumuiba mtoto hadi hapo atakafikisha miaka saba.
  
Tukio la pili la kuiba mtoto.
Alisema tukio hilo lilitokea Novemba 29 mwaka jana 2012, ambapo alifika nyumbani kwao majira ya saa 12 :00 na kumkuta dada wa marehemu kumchukua mtoto akimdanga kuwa anaenda kusenya kuni eneo la jirani.
Aliongeza kuwa baada ya kuona dada wa marehemu anang’ang’ania kwenda wote alimuamuru arudi nyumbani kuchochea moto kwa kuwa kulikuwa kumeinjikwa mboga na kukubali kurudi.
“kwa mujibu wa maelezo ya mwanangu huyu wa kwanza alisema baada kurudi toka ndani, alikuta baba yake huyo ameondoka na mtoto na tuliporudi na kupokea taarifa hizo tulichanganyikiwa na kuanza kuhangaika hovyo” alisema mama wa marehemu.
Mwambenja alisema kuwa baada ya kucha siku ya pili asubuhi yake walienda kutoa taarifa kituo cha polisi cha Kiwira ili waweze kupata msaada wa kumtafuta, huku wakionesha barua ya makubaliano ya awali ya yeye kuwa na haki ya kisheria ya kusimamia malezi ya mwanao hadi afikishe miaka saba.
Alisema baada ya kutoa taarifa hizo kituoni hapo, askari aliyekuwa zamu siku hiyo alimtaka kutoa kiasi cha shilingi 50,000 ili fedha hizo wapewe askari mgambo wa kwenda  kijijini kwa mzazi mwenzake huyo, kwani tayari walikuwa na taarifa kuwa alikuwa amekimbilia huko.
 “Kutokana na hali ngumu ya maisha tulikosa kiasi hicho cha fedha  hivyo suala hilo kubaki bila msaada wa  polisi na pia hatukuweza kwenda kwa kijijini kwao”.
Aliongeza “sababu ya mimi kuwa mzito kuendelea kumfuatilia kijijini kwao kwa mara ya pili ili kujua kama yupo huko na mtoto ilitokana na hofu niliyoijenga, kwani awali tukiwa kwenye ugomvi alitamka maneno ya vitisho kuwa endapo nitaendelea kung’ang’ania kumchukua mtoto pale anapomchukua atakuja kumuua ili tukose wote”.
Hata hivyo mama huyo mzazi wa Debora, alisema kuwa baada ya kuona hali hiyo, aliendelea kuwasiliana na wifi yake , Bupe Mwangoka,ambaye ni dada mkubwa wa mume wake  anayeishi eneo la Isanga  Jijini mbeya, ambaye ndiye alisaidia kwa kiasi kikubwa kubainika kwa  unyama aliofanya.
  
Maisha kabla ya tukio.
Akielezea maisha yao kabla ya kutengana na baadae kuamua kufanya ukatili huo, alisema aliwahi kumtamkia maneno makali wakati akiwa na ujauzito wa miezi nane .
Alisema baada ya kuibuka ugomvi katika kipindi hicho, mwanaume huyo alimtaka kwenda kuiuza mimba ile kwa mwanaume mwingine yeyote atakayempenda ili asije akazaa mtoto ambaye atachanganya damu ya koo hizo mbili.
“Maneno yale katika kipindi hicho sikuyatilia maanani kwani nilifikiri zilikuwa ni hasira, lakini leo hii ndio najua maana ya ile kauli ” alisisitiza Mwambenja.
Hata hivyo alisema inashangaza kwani  kuna wakati tukiwa katika maisha ya kawaida kabla ya yeye kufanya tukio hilo, mara kadhaa alijutia na kuonya juu ya matukio machafu yaliyojitokeza na kusikika ya watu kuuawa au kuondolewa baadhi ya viungo vya miili yao.
Aidha, alieleza mkasa mwingine wa mume wake huyo ni ule wa wao kufukuzwa katika mji wa Kiwira walikokuwa wakiishi awali kwa kufanya shughuli za umachinga.
Alisema walitimuliwa na serikali ya mtaa katika mji huo kutokana na mumewe huyo kutuhumiwa kuiba simu ya mkononi ambapo alipokea kipigo kikali na baadae kufukuzwa.
Kutokana na hali hiyo, mama wa marehemu Debora alisema yote yaliyotokea amemwachia mungu na kwamba kama ingekuwa uwezo wake angeamuru naye anyongwe, hivyo mamlaka husika zitajua cha kufanya.
Kwa upande wake dada wa marehemu Debora, Neema Stevini(5) ambaye ni mtoto wa kufikia wa baba mzazi wa marehemu, akisimulia jinsi mdogo wake alivyoibwa , alisema kuwa anakumbaka mara ya mwisho ilikuwa jioni majira ya saa 12 jioni.
“Nilitaka kwenda nao, lakini baba Debora akaniambia nirudi kuchochea moto ndani na niliporudi nikakuta wameondoka na nilipokimbilia sana siku waona” alisema kwa masikitiko Neema.
Hata hivyo uchunguzi wa Mbeya yetu umebaini kuwa marehemu Debora alifariki dunia siku hiyo ya Novemba 29 mwaka jana, majira ya saa nne usiku baada ya baba yake kufanikiwa kumuiba kutoka nyumbani kwa mama yake.
Inadaiwa kuwa baada ya kufanikiwa kumtorosha baba huyo wa marehemu alitembea kwa mguu umbali wa kilomita 50 kutoka kijiji cha Ibula alikomuiba hadi nyumbani kwake kijiji cha Isange katika kata ya Isange.
Imeelezwa kuwa baada ya kufika nyumbani kwake, baba huyo mzazi wa marehemu alichimba shimo katikati ya sebule na kumchukua mtoto wake huyo akiwa usingizini na kisha kumfukia akiwa hai.
“Mwanaume Yule alikuwa katili sana, kwani baada ya kumfukia alichukua meza ya chakula na kuiweka juu yake huku akiipamba kwa magazeti jambo ambalo lilifanya ndugu zake wasigundue kirahisi” alisema mpasha habari.
Chanzo hicho kilisema baada ya kufanya hivyo aliishi kwa wiki moja na baadae kukimbilia Jijini Mbeya ili watu wasibaini juu kitendo alichofanya na kwamba kila alipohojiwa na ndugu zake alisema mwanae huyo alimuweka kwa rafiki yake Jijini Mbeya.
Hata hivyo baada ya danadana za muda mrefu ndipo dada wa mtuhumiwa huyo aliamua kutoa taarifa jeshi la polisi na kufanikiwa kumkamata akiwa katika harakati za kutorokea wilayani Chunya na alipobanwa alifichua siri ya alipo mwanae kwa kueleza kuwa alimuua na kumfukia ndani kwake.


Joseph Mwaisango
Ezekiel Kamanga
na
Venance Matinya

TAMASHA LA JUMATATU YA PASAKA MBEYA LAFANA NA DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA ATOA SHILINGI MILIONI 8 KUSAIDIA UJENZI WA KITUO CHA WATOTO YATIMA


Mweshimiwa Dk Mary Mwanjelwa  Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mbeya akizindua tamasha la jumatatu ya pasaka lililofanyika katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya
Mwenyekiti wa Kamati Maalumu inayoratibu tamasha la pasaka la kimataifa, Alex Msama akiwashukuru wakazi wa mbeya kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo lililofanyika katika uwanja wa Sokoine Mbeya
Mwenyekiti wa Kamati Maalumu inayoratibu tamasha la pasaka la kimataifa, Alex Msama akipokea msaada wa pesa shilingi milioni 8 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto yatima toka kwa Mweshimiwa mbunge viti maalumu mkoa wa Mbeya Dk Mary Mwanjelwa 
Baadhi ya viongozi mbali mbali wa dini na serikali walihudhuria tamasha hilo
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Solomon Mukubwa akiwatumbuiza wakazi wa Mbeya  
Waimbaji Wa Christ Ambassadors kutoka Rwanda wakiimba kwa furaha katika tamasha hilo

BABA AMZIKA MWANAE WA KIUME WA UMRI WA MIAKA 3 BAADA YA UGOMVI NA MKEWE





MTU mmoja Mkazi wa Kitongoji cha Iponjola Kijiji cha Isange Wilaya ya Rungwe Mkoani hapa anashikiliwa na Jeshi la Polisi akituhumiwa kumzika mwanaye wa kumzaa kwa siri ndani ya nyumba yake.
  
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema lilitokea juzi majira ya saa Saba  mchana baada ya kugundua kuwa  mtoto Debora Riziki (3) kyusa, mkazi wa Iponjola, aligundulika akiwa amefariki baada ya kufukiwa kwenye shimo ndani ya nyumba ya baba yake mzazi.
  
Alimtaja mtuhumiwa kuwa ni Riziki Saidi Mwangoka (27),kyusa,mkulima ,mkazi wa Iponjola na kuongeza kuwa tukio hilo lilifanywa na mzazi huyo Novemba 29, Mwaka 2012.
  
Alisema  chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa kindoa kati ya mtuhumiwa na aliyekuwa mke wake Esther  Msafiri Mwambenja (23),kyusa,mkulima ,mkazi wa Kibumbwe-Kiwira.
  
Kamanda Diwani alisema mgogoro wao ulipelekea wagombee nani aishi na mtoto huyo baada ya wanandoa hao kutengana hivyo Novemba 28, Mwaka 2012 majira ya saa 11 Jioni  mtuhumiwa alimchukua kwa nguvu marehemu kutoka kwa mama yake na kwenda nae kwake kisha kumuua na kumfukia sebuleni ndani ya  nyumba yake.
Alisema  mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na daktari kisha kukabidhiwa ndugu kwa ajili ya kuzikwa ambapo mtuhumiwa amekamatwa na taratibu zinafanywa ili afikishwe mahakamani.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya  anatoa mwito  kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi ili kuepusha matatizo yanayoweza kuepukika.
  
Pia  anatoa rai kwa wanandoa kutatua matatizo na migogoro yao kwa njia ya  kukaa meza ya mazungumzo badala ya kutanguliza hasira na matumizi ya nguvu.

NWAKA MWAKISU AKONGA NYOYO ZA VIJANA MBEYA


Nwaka Mwakisu akiongea na vijana wa Uyole hivi karibuni 
Diwani wa Kata ya Itezi Frank Maemba amesema wanachokifanya Vijana hao ni kutekeleza sera za chama cha mapinduzi inayotaka Vijana waunganishwe kwenye makundi ili iwe rahisi kupatiwa misaada ikiwa ni pamoja na kupunguza uhaba wa ajira kwa vijana.
Timu ya Redio  Bomba fm, 
Timu ya  Veterani ya Uyole 
Timu mbali mbali zilikuwepo uwanjani hapo
Vijana mbali mbali walijitokeza kuchangia damu siku hiyo


BAADHI ya Wananchi na wakazi wa Mkoa wa Mbeya wamepongeza jitihada za Vijana wanaojitolea kusaidia makundi ya watu wasiojiweza na wenye uhitaji kutokana na kufanya hivyo bila kujali itikadi za vyama  wala dini zao.
Kijana anayetajwa kukonga mioyo ya wananchi wa Mbeya kutokana na kusaidia makundi mbali mbali ya Vijana, Yatima na wazee ni Mjumbe wa Mkutano mkuu Taifa kupitia Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mbeya, Nwaka Mwakisu.
  
Wananchi hao wamesema Nwaka Mwakisu amekuwa kivutio kwa Vijana wengi wa kada mbali mbali kutokana na ushiriki wake katika kazi za maendeleo ndani ya Mkoa wa Mbeya ambapo pia amekuwa akiwaunganisha vijana hao kwenye makundi ili waepukane na shughuli zisizofaa katika jamii.
  
Wamesema Mwakisu ameonesha moyo wa tofauti miungoni mwa Vijana Mkoani Mbeya ambapo katika kipindi kifupi cha kuanzia Januari hadi Machi Mwaka huu ameshiriki na kuambatana na vijana kutembelea vituo vya watoto yatima vilivyopo Uyole na Simike Jijini Mbeya.
  
Wakizungumza na Mbeya yetu katika mahojiano maalumu juu na namna Vijana wenye  uwezo wanavyoweza kusaidia makundi mbali mbali katika kuwakomboa kiuchumi  ambapo hawakusita kumtaja Nwaka Mwakisu kuwa ni miongoni mwa vijana wachache wanaojitolea kwa moyo wote.
  
Iddi Ramadhani ni Mwenyekiti wa Bajaji Jiji la Mbeya ambaye alisema Mwakisu amewatembelea mara kadhaa katika kujua wanahitaji nini ili aweze kwasaidia ambapo ameshwasaidia vijana hao Vifaa vya michezo kama vile Jezi, Soksi na Viatu kwa ajili ya timu ya Waendesha bajaji yenye makao makuu Ilemi Jijini Mbeya.
  
Mbali na waendesha bajaji vijana wengine walionufaika na Msaada wa Mwakisu ni timu za Mpira kutoka Uyole katika kata ya Itezi Jijini Mbeya ambao walipatiwa vifaa vya michezo ambavyo ni seti tatu za Jezi na mipira kwa ajili ya mashindano ya Umoja yaliyomalizika hivi karibuni.
  
Nwaka Mwakisu alipotafutwa kuzungumzia maswala hayo alisema binadamu tumeumbwa kwa ajili ya kusaidiana hivyo si vibaya kwa yeye kujitolea kwa watu wenye uhitaji ambapo aliongeza kuwa hafayi hivyo kwa ajili ya kujinufaisha yeye binafsi.
  
Alisema kiu yake ni kuona Vijana wanakuwa na umoja kwani baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiwatumia vijana kuvuruga amani Mkoani Mbeya ambapo baada ya vurugu viongozi hao hawajitokezi kuwasaidia pindi wanapopata madhara kutokana na athari wanazopata katika vurugu hizo.
Kutokana na kuwaunganisha vijana hao katika baadhi ya michezo ambapo vijana hao hupata nafasi pia ya kuchangia damu kutokana na uhitaji wa damu katika michezo iliyomalizika Uyole Jijini Mbeya katika viwanja vya Shule ya Msingi Gombe iliyowahusisha timu ya kituo cha Redio cha Bomba fm, Veterani ya Uyole na vijana wengine.
Mbali na vijana hao kumpongeza Nwaka Mwakisu kwa kujitolea na kuwaunganisha Vijana hao, Diwani wa Kata ya Itezi Frank Maemba alisema wanachokifanya Vijana hao ni kutekeleza sera za chama cha mapinduzi inayotaka Vijana waunganishwe kwenye makundi ili iwe rahisi kupatiwa misaada ikiwa ni pamoja na kupunguza uhaba wa ajira kwa vijana.
  
Hata hivyo wajibu huo umeonekana kutekelezwa zaidi na viongozi vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Mbeya ambao wameonekana kuunga mkono juhudi hizo ambao ni Mjumbe wa Mkutano mkuu taifa(CCM), Charles Mwakipesile ambaye aliwahi kutoa Kompyuta yenye thamani ya Shilingi Laki tano na Nusu(550,000/=) kwa  Vijana wanaoendesha Bajaji Jiji la Mbeya.