Katibu wa
NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwahutubia
wananchi wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya
Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea maeneo hayo na
kuweza kujionea changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo wananchi hao
ikiwa ni pamoja na kutembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya Ujenzi wa
Soko la Kimataifa litakalowanufaisha wakazi wengi wa wilaya hiyo ambao
wako kando kando ya Mto Maragarasi unaopakana na nchi jirani ya
Burundi.Dkt. Migiro pia amewaasa wananchi wa maeneo hayo kuwa na
umoja,mshikamano na upendo ili kuweza kuhimarisha mambo mbali mbali ya
Wilaya.
Katibu wa
NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akihutubia
Mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Buhigwe ambapo ndipo yalipo makao
makuu ya Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya
kutembelea wilaya hiyo jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akicheza ngoma ya asili ya kabila la Waha waliokuja kumpokea.
Wananchi wa Kijiji cha Buhigwe wakimuaga Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro.
Katibu wa
NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na
Viongozi mbali mbali wa CCM katika Kijiji cha Mnanila,Wilayani Buhigwe.
Katibu wa
NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwasalimia
wananchi wa Kijiji cha Mnanila kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya
Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati akiendelea na Ziara yake ya kutembelea Kata
zote zilizopo wilayani humo.
Katibu wa
NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza na
wananchi wa Kijiji cha Buhigwe ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Wilaya
Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea wilaya
hiyo jana.
Katibu wa
NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwapungia
watoto wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya
Buhigwe,Mkoani Kigoma mara baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa
Kijiji hicho jana.
Mmoja wa
wananchi wa Kijiji cha Buhigwe ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Wilaya
Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wakimsikiliza Katibu wa NEC,Siasa
na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro aliekuwa kwenye Ziara ya
kutembelea wilaya hiyo jana.
Mkuu wa Wilaya
ya Buhigwe,Ndg. Gishuli Mbegesi (kulia) akikabidhi Taarifa ya
Utekelezani wa Ilani ya Uchaguzi kwa Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro.
Katibu wa
NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akipokea ripoti
ya Chama Wilaya ya Buhigwe,kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya
Buhigwe,Bi. Bennosa Mjema.Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo,Ndg.
Elisha Bagwanya
Baadhi ya
Wakazi wa Kijiji cha Buhigwe wakimsikiliza Katibu wa NEC,Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro aliekuwa kwenye Ziara ya
kutembelea wilaya hiyo jana.
Katibu wa
NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akicheza ngoma
ya asili ya kabila la Waha sambamba na Bibi Buchiro Edmas Kapina wakati
wa Ziara ya kutembelea wilaya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akilakiwa kwa shangwe na kinamama wa Kijiji cha Kilelema.
Mjumbe wa
Halmashauri ya Kijiji cha Kilelema,Everist Samson akisoma taarifa ya
kijiji kuhusiana na changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi wa
kijiji hizo zikiwemo zile za kuvamiwa na majambazi wanaotoka nchi jirani
ya Burundi.Kijiji hiki kipo mpakani kabisa mwa Tanzania na Burundi kwa
kijiji cha Buhema Mkoani Lutana,nchini Burundi.
Wananchi wa
Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani
Kigoma wakimsikiliza kwa makini Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro (hayupo pichani).
Mwenyekiti wa
Kijiji cha Kilelema,Benedict Samson Mahuta (kulia) akitoa ufafanuzi juu
ya eneo la Soko kwa Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt.
Asha-Rose Migiro (katikati),alietembelea eneo litakalojengwa soko la
Kimataifa katika Kijiji hicho cha Kilelema.
Picha ya Pamoja na Watendaji wa Kijiji cha Kilelema.
Katibu wa
NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro (pili kulia)
akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe,Ndg. Gishuli Mbegesi Charles
(kushoto) kuelekea kwenye eneo la mpaka wa Tanzania na Burundi
unaotenganishwa na sehemu ya Mto Maragarasi.
No comments:
Post a Comment