KESI ya mauaji inayomkabili msanii wa filamu za maigizo nchini,
Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayedaiwa kumuua msanii mwenzake, Steven
Kanumba ‘The Great’ ambayo leo ilitakiwa kutolewa maamuzi ya umri na
Mahakama ya Rufaa imerudishwa mahakama ya Kisutu kuanza upya.
Akitoa
maamuzi hayo, Naibu Msajili wa Mahakama hiyo yenye maamuzi ya mwisho
hapa nchini, Zahra Marume amesema utaratibu uliotumika kuifikisha kesi
hiyo mahakamani hapo ulikuwa na makosa hivyo kuamuru kesi hiyo kurudi
mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
|
No comments:
Post a Comment