Tuesday, 2 April 2013

DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA ASHIRIKI KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA JIJI LA MBEYA NA WALIMBWENDE 30

Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Mbeya kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. Mary Mwanjelwa alipokuwa akiongoza shughuli za usafi wa Mazingira zilizofanywa na walimbwende 30 walioko kwenye kambi ya kumtafuta Mwanamitindo wa Nyanda za Juu kusini.
Hapa mweshimiwa mbunge akiwachekesha walimbwende hao wakati wakifanya usafi kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani 
Hapa mweshimiwa mbunge akiwa na walimbwende wakifanya usafi kituo cha mabasi cha kabwe jijini Mbeya
Mweshimiwa mbunge Dk Mary mwanjelwa akihutubia wananchi na walimbende waliomuunga mkono katika ufanyaji wa usafi katik jiji la Mbeya  hapa ni eneo la kabwe



WALIMBWENDE wanaoshiriki vinyang’anyiro mbali mbali hapa nchini na nje ya nchi wameaswa kulinda maadili na utamaduni wa Tanzania ili kuhakikisha kuwa Watanzania wanaheshimika.
Mwito huo ulitolewa  na Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Mbeya kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. Mary Mwanjelwa alipokuwa akiongoza shughuli za usafi wa Mazingira zilizofanywa na walimbwende 30 walioko kwenye kambi ya kumtafuta Mwanamitindo wa Nyanda za Juu kusini.
  
Mwanjelwa aliongoza usafi huo kuanzia Stendi kuu ya Mabasi yaendeyo Mikoani, Stendi ya Daladala ya Mwanjelwa na kuishia Stendi kuu ya Daladala ya Kabwe Jijini Mbeya huku akiongozana na Walimbwende hao.
  
Mbunge huyo alisema lengo la kufanya usafi ni kutokana na mtoto wa kike kuwa ndiye mwanaharakati anayetakiwa kuwa mfano katika usafi wa mazingira ambayo husaidia kujenga afya nzuri na kuimarisha uchumi wa eneo husika.
  
Alisema Mtoto wa kike ndiye anayetakiwa kuwamstari wa mbele katika kuhakikisha anatengeneza mazingira masafi na mazuri kwa ajili ya kujenga afya bora na kuwa mfano wa kuigwa katika jamii.
  
Aidha aliwasihi walimbwende hao kuheshimu mila na utamaduni wa Mtanzania pindi wanapokuwa wakishiriki mashindano hayo na siyo kuiga tabia ambayo siyo nzuri na inayoitambulisha vibaya nchi ya Tanzania.
  
Alisema suala la ulimbwende ni suala la utamaduni na sanaa hivyo linatakiwa kuungwa mkono na jamii yote na siyo kuwakatisha tama waandaaji.
  
Kwa upande wake mwandaaji wa mashindano hayo Bahati Mwakalinga alisema Jumla ya Walimbwende 30 watachuana jukwaani kumtafuta Mwanamitindo wa Nyanda za Juu kusini katika mashindano yakayofanyika Machi 30, Mwaka huu katika Ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya.
  
Alisema washiriki hao wametoka katika Mikoa ya Mbeya, Katavi, Rukwa, Njombe, Iringa na Ruvuma ambapo alitaja viingilio kuwa ni Shilingi 10,000/=, 25,000/= kwa Vip  na 50,000/= kwa ajili ya meza yenye watu watano.
  
Alisema mashindao hayo yameandaliwa na kampuni ya Tanzania Youth Arise kutoka Dar Es Salaam ambayo imekuwa akiandaa mashindao kama hayo kwa miaka mitano mfulululizo kwa mikoa ya Dar Es Salaam na Pwani ambapo kwa kanda ya Nyanda za Juu Kusini ni mara ya kwanza.
Aliongeza kuwa washindi watano katika kinyanyanyiro hicho wataenda kushiriki mashindano mengine ya dunia yaitwayo Miss Universe pamoja na zawadi mbali mbali ambazo hakuweza kuzitaja.
Walimbwende hao kwa hivi sasa wameweka kambi katika Hoteli ya Manyanya iliyoko Forest Mpya Jijini Mbeya.

No comments: