Wednesday, 1 May 2013
MHANDISHI WA MAJI NJOMBE AMEKUTWA AMEFARIKI KATIKA KISIMA CHA MAJI
..
Kikosi cha Zima moto na uokoaji cha Halmashauri ya mji wa Njombe kwa kushirikiana na wananchi wakitoa mwili wa Mhandisi wa Maji katika Halmashauri ya Mji wa Njombe Abdalah Mgambo baada ya kutumbukia kwenye kisima hicho jana katika Uwanja wa ukumbi wa Turbo Mjini Njombe.
Mwili wa Eng.Abdalah Mgambo ukionekana kwa umbali kwenye gari la Polisi ukipelekwa hospitali Kibena kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.
Wa pili kushoto ni Mhandisi wa Maji Halamshauri ya Mji wa Njombe Eng.Abdalah Mgambo enzi za uhai wake wakati wa Kilele cha Wiki ya Maji March 22 mwaka huu katika kijiji cha Igominyi.
Marehemu Abdalah Mgambo enzi za Uhai wake akisoma taarifa ya Hali ya maji katika halmashauri ya Mji wa Njombe mwezi machi 22 mwaka huu wakati wa kilele cha wiki ya Maji Igominyi Njombe.
Taarifa toka eneo la Tukio zinasema kuwa marehemu Abdalah Mgambo alikuwa katika Baa yake eneo la Ukumbi wa Turbo Mjini Njombe kisha akamuaga mke wake kwamba anatoka nje kujipumzisha kwenye gari lake majira ya Saa Moja jioni jana April 30 akatoweka ghafla na kisha Kadi yake ya Benki ya NMB Ilikutwa nje ya Kisima cha Maji kilichopo katika uwanja wa Ukumbi wa Turbo Mjini Njombe.
Subscribe to:
Posts (Atom)