Vijana mbali mbali walijitokeza kuchangia damu siku hiyo
BAADHI ya Wananchi na wakazi wa Mkoa wa Mbeya
wamepongeza jitihada za Vijana wanaojitolea kusaidia makundi ya watu
wasiojiweza na wenye uhitaji kutokana na kufanya hivyo bila kujali itikadi za
vyama wala dini zao.
Kijana anayetajwa kukonga mioyo ya wananchi wa
Mbeya kutokana na kusaidia makundi mbali mbali ya Vijana, Yatima na wazee ni
Mjumbe wa Mkutano mkuu Taifa kupitia Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
(UVCCM) Mkoa wa Mbeya, Nwaka Mwakisu.
Wananchi hao wamesema Nwaka Mwakisu amekuwa
kivutio kwa Vijana wengi wa kada mbali mbali kutokana na ushiriki wake katika
kazi za maendeleo ndani ya Mkoa wa Mbeya ambapo pia amekuwa akiwaunganisha
vijana hao kwenye makundi ili waepukane na shughuli zisizofaa katika jamii.
Wamesema Mwakisu ameonesha moyo wa tofauti
miungoni mwa Vijana Mkoani Mbeya ambapo katika kipindi kifupi cha kuanzia
Januari hadi Machi Mwaka huu ameshiriki na kuambatana na vijana kutembelea
vituo vya watoto yatima vilivyopo Uyole na Simike Jijini Mbeya.
Wakizungumza na Mbeya yetu katika mahojiano
maalumu juu na namna Vijana wenye uwezo wanavyoweza kusaidia makundi
mbali mbali katika kuwakomboa kiuchumi ambapo hawakusita kumtaja Nwaka
Mwakisu kuwa ni miongoni mwa vijana wachache wanaojitolea kwa moyo wote.
Iddi Ramadhani ni Mwenyekiti wa Bajaji Jiji la
Mbeya ambaye alisema Mwakisu amewatembelea mara kadhaa katika kujua wanahitaji
nini ili aweze kwasaidia ambapo ameshwasaidia vijana hao Vifaa vya michezo kama
vile Jezi, Soksi na Viatu kwa ajili ya timu ya Waendesha bajaji yenye makao
makuu Ilemi Jijini Mbeya.
Mbali na waendesha bajaji vijana wengine
walionufaika na Msaada wa Mwakisu ni timu za Mpira kutoka Uyole katika kata ya
Itezi Jijini Mbeya ambao walipatiwa vifaa vya michezo ambavyo ni seti tatu za
Jezi na mipira kwa ajili ya mashindano ya Umoja yaliyomalizika hivi karibuni.
Nwaka Mwakisu alipotafutwa kuzungumzia maswala
hayo alisema binadamu tumeumbwa kwa ajili ya kusaidiana hivyo si vibaya kwa
yeye kujitolea kwa watu wenye uhitaji ambapo aliongeza kuwa hafayi hivyo kwa
ajili ya kujinufaisha yeye binafsi.
Alisema kiu yake ni kuona Vijana wanakuwa na
umoja kwani baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiwatumia vijana kuvuruga amani
Mkoani Mbeya ambapo baada ya vurugu viongozi hao hawajitokezi kuwasaidia pindi
wanapopata madhara kutokana na athari wanazopata katika vurugu hizo.
Kutokana na kuwaunganisha vijana hao katika
baadhi ya michezo ambapo vijana hao hupata nafasi pia ya kuchangia damu
kutokana na uhitaji wa damu katika michezo iliyomalizika Uyole Jijini Mbeya katika
viwanja vya Shule ya Msingi Gombe iliyowahusisha timu ya kituo cha Redio cha
Bomba fm, Veterani ya Uyole na vijana wengine.
Mbali na vijana hao kumpongeza Nwaka Mwakisu kwa
kujitolea na kuwaunganisha Vijana hao, Diwani wa Kata ya Itezi Frank Maemba
alisema wanachokifanya Vijana hao ni kutekeleza sera za chama cha mapinduzi
inayotaka Vijana waunganishwe kwenye makundi ili iwe rahisi kupatiwa misaada
ikiwa ni pamoja na kupunguza uhaba wa ajira kwa vijana.
Hata hivyo wajibu huo umeonekana kutekelezwa
zaidi na viongozi vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Mbeya ambao wameonekana
kuunga mkono juhudi hizo ambao ni Mjumbe wa Mkutano mkuu taifa(CCM), Charles
Mwakipesile ambaye aliwahi kutoa Kompyuta yenye thamani ya Shilingi Laki tano
na Nusu(550,000/=) kwa Vijana wanaoendesha Bajaji Jiji la Mbeya.
|
No comments:
Post a Comment